Friday, 21 August 2015

Utafiti Wambeba Magufuli Urais 2015



Utafiti waonyesha Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuwa Rais Na Mwandishi Wetu WAKATI kesho Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikitarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Taasisi ya Maendeleo, Vijana, Uongozi na Utawala Bora(YDG) imetoa utafiti na kuonyesha mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli anaongoza. Utafiti huo ulitolewa jana mjini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Christopher Maganila, ambaye alisema katika utafiti walioufanya kuwa endapo uchaguzi mkuu ungefanyika leo, Dk Magufuli angeshinda nafasi hiyo. Alisema matokeo hayo, yanaonyesha Dk. Magufuli angeshinda kwa asilimia 45, huku mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa angekuwa na asilimia 10.5, huku asilimia 35 wakisema hawajaamua mgombea gani anaweza kuwa Rais kwa kuwa ni bado mapema mno. Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa wagombea wengine wangepata asilimia 0.1 hadi 5 huku asilimia 8 wakionekana wakisema hawajui ni mtu gani anafaa kuwa Rais kati ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo. “Huu ni utafiti huru na umefanikiwa kufika kwenye kila mkoa lakini kwa wilaya moja kwa kuwa tumeamua kuwahi ili kuona mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuchagua mgombea wanayemhitaji,’’alisema. Hata hivyo, Katibu huyo mtendaji alisema sababu nyingi walizoonekana kuzitoa wananchi kuwa Dk. Magufuli atakuwa mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa wa kufanya kazi endapo akipewa ridhaa. Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema anaamini uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa huru na haki kwa kuwa wananchi wameonekana kuwa na mwamko katika kuchagua kiongozi atakayewaongoza.

Source: Jamii Forums

Sunday, 21 September 2014

HABARI MOTO: SAKATA LA IPTL NA ESCROW KAFULILA AANZA KUUMBUK...

HABARI MOTO: SAKATA LA IPTL NA ESCROW KAFULILA AANZA KUUMBUK...: IPTL yang’ara  A/Mashariki Sasa kusambaza umeme MW 2000 Kenya  Kafulila aumbuka kwa kusema Sethi Hatakiwi Kenya                ka...

Tuesday, 16 September 2014

SAKATA LA IPTL NA ESCROW CAG ANATUMIKA VIBAYA








Katika hali isoyotarajiwa na wengi, hivi sasa imejidhirisha wazi kwamba CAG anatumika kisiasa ili kuandaa ripoti ambayo itawafuraisha wapinzani wa kibiashara wa IPTL. 

Taarifa tulizonazo ni kwamba CAG amekuwa akiandaa ripoti ya ukaguzi wake huku akiwa bega kwa bega na wale waliyoshiriki kulilalamikia swala hili ambao ni KAFULILA&CO.

Mpaka hadi sasa haijulikani anatumika kwa maslahi ya nani?

Nikweli kwamba CAG hana mahusiano mazuri na baadhi ya maafisa wa serekali,je kuna haja ya kutumika kuwahujumu IPTL na serekali?

kwa nini alazimeshe kusema mchakato ESCROW ni wakifisadi wakati watu wamelipwa hela zao baada ya kuuza umeme TANESCO?

Je walitaka umeme uchukuliwe bure?

Au IPTL ni mjomba wa TANESCO mpaka iwe hivyo?

Naomba kuwasirisha kwa masikitiko makubwa

Saturday, 13 September 2014

MBUNGE WA MPENDAE AIDHARIRISHA CHADEMA MBELE YA AFISA MWANDAMIZI WA POLISI



 Mbunge wa jimbo la Mpendae CCM Salim Turki amekidharirisha, kukifedhehesha, na kukitukana Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kusema kwamba ni chama cha watu wasio na akili ,wasio na misingi na kwamba CCM inaweza kuwafanya lolote na wasifanye kitu.

Mbunge huyo amewadharirisha CHADEMA mbele ya kikao cha usuluhishi baina ya Upande wao na wenzao kilichofanyika Central polisi hivi karibuni,mbele ya Maafisa waandamizi wa polisi,ambapo aliitwa pamoja na upande wa pili ambao wanaopingana kujadili namna ya kutatua mgogoro wao.

Aliwafananisha anaopingana nao sawa na CCM wanavyowanyanyasa CHADEMA bungeni na kwamba sauti yao haina pa kusikika na wasio na lolote wala chochote.
Hii ni dharau kubwa kufanywa na Mbunge kwa CHADEMA.

CHADEMA MPOOO!

ONA VIDEO HII






 SOURCE YA HABARI NI JAMII FORUM


http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/723612-mbunge-turki-wa-mpendae-aidharirisha-chadema.html#post10586291